Saturday, June 25, 2011

Shilole, Tafu, wana 'Sikitiko la Mahaba'


MSANII wa filamu ambaye pia ni mwanamuziki, Ramadhani Ally 'Tafu' anatarajia kufyatua filamu yake ya kwanza binafsi iitwayo 'Sikitiko la Mahaba' ambaye atamshirikisha mwanadada anayekuja juu katika fani hiyo, Zena Mohammed 'Shilole'.
Akizungumza na mtandao huu, Tafu, aliyewahi kuwa rapa wa bendi ya Extra Bongo, alisema kazi yake hiyo inayohusika na simulizi ya mapenzi, itawashirikisha pia wasanii wengine wakali kama,  Hisani Muya 'Tino', Ndende, Osela na Tiko.
"Baada ya kutumika kwenye filamu za wengine, hatimaye nimeandaa kazi yangu binafsi ambayo inatarajiwa kurekodiwa wiki ijayo ambayo nitawashirikisha  wakali kama Shilole, Tino, Ndende, Osela na wengineo," alisema.
Aliongeza mara baada ya kazi hiyo kukamilika ataingia tena 'chimbo' kwa ajili ya kufyatua kazi nyingine mbili ambazo tayari ameshaziandaa zilizopewa majina ya 'Boniface' na 'Usinue' atakazoandaa kwa ushirikiano na Shilole na Ndende.
Tafu aliyeuza sura katika kazi mbalimbali kama 'Sawaka', 'Pooja', 'My Darling', 'Paparazi', 'Sikio la Kufa', 'Mahabati', 'The Game of Love', 'Betraya' na nyingezo, alisema ana imani kazi hizo tatu zitamweka katika matawi ya juu kutokana na jinsi simulizi zake zilivyo.
Katika hatua nyingine, msanii nyota wa filamu za vichekesho, Tumaini Martin 'Matumaini' anayetamba sokoni kwa sasa na filamu yake binafsi ya 'Nichakachue Nikuchachue' yupo mbioni kufyatua kazi nyingine mpya iitwayo 'Tifutifu' ambayo imesharekodiwa.
Akizungunza na blogs hii,, Matumaini aliyeibuliwa kwenye sanaa na kundi la Kaole Sanaa, alisema katika kazi hiyo mpya ameshirikiana na waigizaji mahiri wa uchekeshaji kama alivyofanya katika kazi yake ya kwanza inayotamba sokoni.

No comments:

Post a Comment